• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa sukari watakiwa kuendelea kuagiza bidhaa hiyo

    (GMT+08:00) 2019-02-22 19:12:04

    Waziri wa Kilimo wa Tanzania Bw Japhet Hasunga ametengua kauli yake kuhusu sukari, baada ya kuwataka kuendelea kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi tofauti na zuio lake la awali.

    Waziri huyo alitoa zuio hilo Februari 12 aliposema kuwa Serikali haitatoa vibali kwa wazalishaji wa sukari nchini humo kwa kuwa kufanya hivyo husababisha wajikite zaidi katika kuagiza badala ya kuzalisha.

    Kampuni za sukari za TPC, Kilombero, Kagera na Mtibwa zitapewa vibali vya kuagiza sukari kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya tani 215,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida kwa mwaka.

    Alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya Serikali kufanya tathmini na kuridhishwa na mipango mikakati iliyowekwa na kampuni hizo za kuongeza uzalishaji wa sukari hadi kufikia tani 345,000 kwa mwaka.

    Sukari ilipanda bei kwa kasi mwaka 2016 baada ya Serikali kutangaza bei elekezi ya bidhaa hiyo.

    Hata hivyo, Serikali ilisema kasi hiyo ya kupanda kwa bei ya sukari ilitokana na wafanyabiashara kuificha na hivyo kuanza msako katika maghala, hali iliyosababisha bidhaa hiyo kuendelea kupanda bei.

    Tanzania kwa sasa inazalisha tani 300,000 za sukari kwa mwaka, wakati mahitaji ni tani 670,000 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako