• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri akanusha kuhusika kwenye sakata ya ufisadi Kenya

    (GMT+08:00) 2019-02-22 19:15:15

    Waziri wa Utalii wa Kenya Bw. Najib Balala amejitetea mbele ya Kamati ya Bunge kuhusu Michezo, Utalii na Utamaduni, kuhusiana na madai ya ufisadi katika wizara yake.

    Wizara hiyo inadaiwa kupunja Sh100 milioni katika hafla ya muungano wa Maajenti wa Usafiri kutoka Amerika (ASTA) iliyoandaliwa Jijini Nairobi 2017.

    Waziri huyo pamoja na baadhi ya maafisa katika wizara yake tayari wamehojiwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusiana na sakata hiyo, ambapo wizara inalaumiwa kuwa ilitoa tenda ya hafla hiyo ya ASTA kuandaliwa bila mashirika mengine kupewa fursa.

    Lakini akiwa mbele ya kamati hiyo, Bw Balala alikosoa wanaodai kuwa hafla hiyo ilihusisha utoaji tenda, akisema ilikuwa hali ya Kenya kupigania kuwa mwenyeji wake na kuwa iliinua utalii nchini.

    Alisema ijapokuwa uchunguzi kuhusu sakata ya ASTA umekuwa ukiendelezwa dhidi ya maafisa wa wizara yake kwa miezi sita iliyopita, baada ya jina lake kutajwa baadhi ya watu wameingiza siasa katika suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako