• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini watoa msaada wa dawa za kukinga malaria

    (GMT+08:00) 2019-02-22 19:37:41

    Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa msaada wa dawa za kukinga malaria zenye thamani ya dola za kimarekani 744,000 ili kuimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kupambana na malaria.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini He Xiangdong amesema, dawa hizo zitaongeza uwezo wa Sudan Kusini kukabiliana na mlipuko wa malaria na kuboresha sekta ya afya ya nchi hiyo. Pia amesema China itaendelea kuiunga mkono sekta ya afya ya Sudan Kusini kupitia kuendelea uwezo wa wahudumu wa afya.

    Waziri wa fedha wa Sudan Kusini Salvatore Garang ambaye alipokea msaada huo hapo jana, ameisifu China kwa juhudi zake katika kuiunga mkono nchi hiyo. Ameongeza kuwa Sudan Kusini inataka kuimarisha uhusiano wa pande mbili na China katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, maendeleo na elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako