• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kombe la EFL: Man City Bingwa baada ya kuipiga Chelsea

  (GMT+08:00) 2019-02-25 08:15:17

  Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu kwa fainali ya EFL Cup kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City kujua timu gani itakuwa Bingwa, mchezo huo ulimalizika kwa rekodi nyingine kuvunjwa baada ya Chelsea iliyo chini ya kocha Maurizio Sarri na Man City iliyo chini ya kocha Pep Guardiola kushindwa kupata mshindi kwa dakika 90.

  Mchezo huo haukuwa rahisi kama wengi walivyofikiri na hatimae kulazimika kwenda dakika 120 ila mambo yalikuwa magumu kwa pande zote mbili, ndipo mikwaju ya penati ilipoamua timu gani iwe bingwa, Chelsea licha ya kuwa imara na kudhibiti mashambulizi ya Man City lakini walijikuta wakipoteza kwa penati 4-3.

  Hii ndio mara ya kwanza kwa mchezo wa fainali ya EFL Cup kuchezwa dakika 120 pasipo kupatikana Bingwa toka mwaka 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako