• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zinatakiwa kuendelea kufanya juhudi ili kupanua maslahi yao zaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-25 10:43:43

    Duru ya saba ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani yalimalizika tarehe 24 Jumapili mjini Washington. Kwenye mazungumzo hayo ya siku nne, pande mbili zimekubaliana kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili walipokutana nchini Argentina, na kupata maendeleo halisi juu ya masuala ya uhamisho wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki ya ubunifu, vizuizi visivyo ushuru, sekta za huduma na kilimo, kiwango cha ubadilishanaji wa fedha na mengineyo. Wakati huohuo, rais Donald Trump wa Marekani amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ataahirisha mpango wa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zitakazoingizwa Marekani uliopangwa kuanza tarehe mosi mwezi Machi.

    Matokeo haya mazuri yameonesha kuwa pande zote mbili zinajitahidi kupanua maslahi yao ya pamoja, ambapo China imeahidi kuongeza uagizaji wa bidhaa za kilimo, nishati, na huduma kutoka Marekani, jambo ambalo limetatua ufuatiliaji wa Marekani juu ya pengo la biashara kati yake na China, bali pia limekidhi mahitaji ya wachina juu ya maisha bora na kusaidia kuboreshwa kwa muundo wa kiviwanda nchini China.

    Kwa mfano wa bidhaa za kilimo, waraka uliotolewa wiki iliyopita na baraza la mawaziri la China umesisitiza kuhakikisha usalama wa chakula, na pia kuongeza uagizaji bidhaa za kilimo zenye mahitaji makubwa ndani ya nchi, na soya ni moja ya bidhaa hizo, na kila mwaka asilimia 90 ya soya inaagizwa kutoka nje, na kupanua uagizaji soya kutoka Marekani kunaweza kuziba pengo la mahitaji ndani na soko la soya la China ambalo linaagiza asilimia 57 za soya inayouzwa nje na Marekani, ni muhimu sana kwa Marekani.

    Katika suala la muundo wa kibiashara kati ya China na Marekani, madai mengi yaliyotolewa na Marekani isipokuwa yale yanayohusu maslahi ya taifa ya China, itikadi na usalama wa taifa, yanalingana na kazi zinazofanywa na China katika kuimarisha mageuzi, kufungua mlango na kutimiza maendeleo mazuri ya uchumi.

    Hivi sasa nchi hizo mbili zimeanza mazungumzo kuhusu waraka wa makubaliano yatakayofikiwa, kipindi ambacho kitakuwa kigumu zaidi. Ili kulinda maslahi ya nchi, wajumbe wa biashara wa pande hizo mbili hakika watajadili kwa kina na neno kwa neno maudhui ya waraka huo, kwa hivyo kuahirisha mpango wa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China kutazipa pande hizo mbili muda zaidi wa kupanua maslahi yao ya pamoja, na kufikia makubaliano ya kuzinufaisha pande zote mbili.

    China itaendelea kufanya mazungumzo kwa dhati na jitihada katika kazi zijazo, na kutarajia Marekani kuelewana nayo na kufanya juhudi kwa pamoja. Wakati huohuo, China itatekeleza mambo yake kwa kasi iliyopangwa, kuimarisha mageuzi na kufungua mlango, na kukabiliana na mabadiliko ya nje katika hali ya utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako