• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bandari mpya kujengwa Kampala

  (GMT+08:00) 2019-02-25 20:00:09
  Mamlaka ya kulinda mazingira nchini Uganda imeidhinisha ujenzi wa bandari mpya ya Kampala katika wilaya ya Wakiso.

  Afisa wa ngazi ya juu wa mamlaka hiyo Leilah Akello amesema udongo wa sentimita milioni moja za ujazo utatolewa kwenye eneo hilo.

  Mradi huo pia utachukua eneo la ekari 465 za ardhi na hivyo watu wanaoishi kwenye eneo hilo watahama.

  Serikali hata hivyo imesema haitawafidia watu hao kwani walijenga kwenye ardhi ya serikali na eneo la msitu.

  Bandari hiyo mpya itaunganisha huduma za usafiri kati ya Kampala na Tanzania na kupunguza gharama za uchukuzi kati ya nchi hizo mbili.

  Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa bandari hiyo, eneo huru la biashara na maneo ya kuegesha meli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako