• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbio za Baiskeli: Merhawi wa Eritrea ashinda hatua ya pili

  (GMT+08:00) 2019-02-26 08:07:23

  Merhawi Kudus kutoka Eritrea jana amefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza kwenye hatua ya pili ya mbio za baiskeli za Rwanda.

  Kudus alitumia saa 3 na dakika 2 katika umbali wa kilomita 120 kuanzia mji wa Kigali hadi mjini Huye.

  Mshindi wa pili wa hatua hiyo alikuwa Kasperkiewicz Przmyslaw kutoka Poland, mshindi wa tatu akiwa ni Girmy Hailu Biniam wa Eritrea, huku bingwa mtetezi wa michuano hiyo Samuel Mugisha akishika nafasi ya tisa.

  Mbio hizo zinaendelea leo kwa waendesha baiskeli hao kushindana katika hatua ya tatu yenye umbali wa kilomita 213 kuanzia mjini Huye hadi katika mji wa Rubavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako