• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Mauzo ya nje yaongezeka kwa asilimia 5.1

  (GMT+08:00) 2019-02-26 20:27:11

  Dhahabu,samaki,mafuta na mahindi vimeongoza katika orodha ya mauzo ya nje Uganda ya mwaka 2018,na kuongeza jumla ya mapato kwa asilimia 5.1.

  Kulingana na takwimu kutoka Benki ya Uganda (BoU) zilizotolewa mwezi huu,mapato ya mauzo ya nje ya nchi hiyo kufikia mwisho wa mwaka 2018 yalikuwa $3.6b (Ushs13.2trilioni), kutoka $3.4b (Ushs12.5 trillion) zilizopatikana mwaka 2017.

  Kwa mara nyingine tena dhahabu ndio bidhaa iliyoongoza kwa kuipatia Uganda mapato ya $514.8m (Ushs1.8 trillion).

  Ripoti hiyo ya Benki ya Uganda inaonyesha kuwa jumla ya kilo 13,216 za dhahabu ziliuzwa nje ya nchi,kutoka 10,380 zilizouzwa mwaka 2017.

  Wachambuzi wa mauzo ya nje wanasema kuongezeka kwa mauzo ya dhahabu kumechangiwa na kiwanda cha kusafisha bidhaa hiyo cha Africa Gold Refinery cha Entebbe kilichoanzishwa mwaka 2014.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako