• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa stakabadhi ghalani wawanufaisha wakulima wa kakao Mbeya,Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-02-26 20:29:50

  Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,mkoani Mbeya ,imesema mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye uuzaji wa zao la kakao umesaidia kupunguza idadi ya wafanyabiashara waliokuwa wakinunua zao hilo moja kwa moja kutoka kwa wakulima na kukwepa ushuru.

  Halmashauri hiyo imesema mfumo huo sasa umesaidia ongezeko la kampuni zinazonunua zao hilo kwenye Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Kyela na kurejesha sehemu ya faida kwa wananchi.

  Akizungumza jana jijini Mbeya,Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo,Lucy Mganga,alisema jitihada za kuhamasisha wakulima kuijunga kwenye vyama vya ushirika zimezaa matunda na kila mkulima sasa ananufaika na zao hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako