• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya kuzalisha umeme ya KenGen yasaini mkataba wa kuzalisha nishati ya mvuke Ethiopia wa thamani ya $76.8mn

  (GMT+08:00) 2019-02-26 20:30:11

  Kampuni kubwa ya kuzalisha umeme Kenya ya KenGen imeshinda kandarasi ya kuchimba vizima vya nishati ya mvuke nchini Ethiopia.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KenGen Rebecca Miano na mwenzake wa kampuni ya Umeme ya Ethiopia (EEP) Abraham Belamy walitia saini mkataba huo wikendi iliyopita.

  Mradi huo unahusisha uchimbaji ,uendeshaji pamoja na matengenezo ya visima vya nishati ya mvuke katika eneo la Aluto,nchini Ethiopia.

  Mradi utatekelezwa kwa awamu mbili.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KenGen Rebecca Miano jana alisemna mkataba huo utapanua mkakati wa kampuni hiyo wa kuingiza mapato.

  Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mkopo wa $76.8 milioni (Sh7.6 billion) kwa serikali ya Ethiopia.

  KenGen inaendesha vituo vya nishati ya mvuke nchini Kenya,huku kituo cha Olkaria 1 kikiwa kituo cha kwanza cha nishati ya mvuke barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako