• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara: Kituo kinachofuata ni Shinyanga yasema Klabu ya Simba

  (GMT+08:00) 2019-02-27 08:29:22

  Kamwene, Timu ya Lipuli FC imeshindwa kuonyesha makucha yake katika uwanja wa nyumbani mjini Iringa ilipokubali kipigo cha magoli 3-1 dhidi ya Simba ya Dar es Salaam kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa jana.

  Magoli ya Clatous Chama dakika ya 6 na 44 ya mchezo na la Kagere dakika ya 57 zimetosha kuiongeza Simba alama katika msimamo wa ligi hiyo. Goli la kufutia machozi la wana Paluhengo Lipuli lilifungwa dakika ya 18 na mshambuliaji wake Paul Nonga.

  Simba sasa inaelekea mjini Shinyanga kukabiliana na Stand United kabla ya kurejea Dar es Salaam kujiandaa na safari ya kuwafuata AS Jaoura ya Algeria katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako