• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Waziri wa kilimo Tanzania ataka bajeti kubwa kwenye sekta hiyo

  (GMT+08:00) 2019-02-27 19:53:11

  Waziri wa Kilimo wa Tanzania Japhet Hasunga, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa nchi za Afrika, kutenga bajeti ya kutosha kwa wataalamu wanaofanya utafiti katika kilimo.

  Hasunga alisema hayo katika mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini Arusha wa kuzindua mradi wa Avisa, uliolenga kueneza na kuhimiza teknolojia za mbegu bora za mazao ya jamii ya mikunde na nafaka.

  Alisema nchi za Afrika zimetakiwa kutenga fedha nyingi, kwenye bajeti zao katika sekta ya kilimo ili kuwawezesha watafiti kuleta matokeo chanya na kwamba hatua hiyo itasaidia upatikanaji wa mbegu bora zitakazowasaidia wananchi kuongeza kipato na kuondokana na umaskini.

  Alipongeza mkutano huo kufanyika nchini na kukutanisha watafiti, wataalamu na wasomi kutoka nchi saba za Afrika. Nchi hizo ni Tanzania, Mali, Burkina Faso, Nigeria, Ghana, Uganda na Ethiopia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako