• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC: Biashara huru bado haijafanikiwa EAC

    (GMT+08:00) 2019-02-27 19:53:26

    Baraza la Biashara la Mashariki ya Afrika (EABC) limesema maafisa wake wameanza kutembea nchi zote wanachama wa EAC kuelewa kwa nini bidhaa na huduma hazisafirishi huru kama inavyootakiwa.

    Akizungumza katika mkutano wa wakurugenzi afisa mkuu wa EABC, bwana Peter Mathuki, alisema wanataka kuelewa kwa nini bidhaa na huduma zinakumbana na vikwazo ilhali kuna soko la kikanda bila vikwazo vya biashara.

    Alisema biashara miongoni mwa nchi za EAC ni asilimia 16, SADC asilimia 47, huku Umoja wa Ulaya ikiwa ni zaidi ya asilimia 70.

    Uchunguzi wa vizuizi visivyo na ushuru ambavyo hupunguza harakati za bidhaa zimeripotiwa kote kwenye kanda hiyo huku baadhi ya nchi zikizuia bidhaa kutoka kwa nchi nyingine wanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako