• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Benki ya dunia imeipa Tanzania zaidi ya shilingi trilioni 2 ndani ya miaka 3

  (GMT+08:00) 2019-02-27 19:53:43

  Serikali ya Tanzania imesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais John Magufuli, Benki ya Dunia imeshatoa zaidi ya shilingi trilioni mbili kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

  Fedha hizo zimetumika katika miradi mitatu ya uendelezaji wa majiji, miji na Jiji la Dar es Salaam katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, vituo vya mabasi, madampo na masoko katika mikoa mbalimbali nchini.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, aliyaeleza hayo jana alipoongozana na maofisa kutoka Benki ya Dunia, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam inayotekelezwa na wizara yake katika manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke.

  Akiwa katika Manispaa ya Temeke alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Buza, Jafo alisema Benki ya Dunia imesaidia utekelezaji wa miradi itakayowezesha kukuza uchumi wa wananchi na maendeleo ya taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako