• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: FIFA yamfungia maisha mwamuzi wa Tanzania kutokana na rushwa na upangaji matokeo

  (GMT+08:00) 2019-02-28 08:11:42

  Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka duniani (FIFA) chini ya mwenyekiti wake, Vassilios Skouris imemfungia maisha mwamuzi wa zamani wa kimataifa na Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT), Oden Charles Mbaga kutojihusisha na masuala ya soka ngazi ya kitaifa na kimataifa baada ya kutiwa hatiani kwa rushwa na upangaji matokeo.

  Afisa habari na mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema mjini Dar es Salaam kwamba baada ya uchunguzi uliofanyika kuanzia Julai 11 mwaja jana, Mbaga amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye upangaji wa matokeo ikiwa ni kinyume na kanuni za maadili za FIFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako