• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufisadi na ukosefu wa usalama vikwazo kwa uwekezaji Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:45:22

    Shirika la Control Risks limetaja ufisadi, ukosefu wa usalama na mazingira duni ya kibiashara kama changamoto kuu za uwekezaji katika kanda ya Afrika mashariki.

    Kutokana na changamoto hizo, shirika hilo limesema baadhi ya kampuni ambazo huwekeza mitaji mikubwa katika sekta kama vile mafuta na uchimbaji madini, zinaepuka uwekezaji au kuchukua tahadhari nyingi kabla ya kuwekeza.

    Ufisadi unajitokea katika nchi hizo hasa wakati wa kupata vibali na leseni husika za kuanza uwekezaji.

    Kulingana na shirika hilo Kenya iko katika nafasi ya 143 kati ya nchi 180 kwenye ufisadi, Uganda nafasi ya 151 nayo Tanzania ikiwa nafasi ya 103.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako