• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Utoaji wa leseni kwa kampuni za madini wakamilika

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:46:36

    Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini inakamilisha taratibu za utoaji wa leseni kwa migodi mikubwa ambazo hazijawahi kutolewa nchini, huku migodi hiyo ikitarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.

    Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, alipokutana na viongozi wa jumuiya ya watendaji wakuu wa taasisi binafsi ofisini kwake, jijini Dodoma.

    Kuhusu Sheria ya Madini ya Mwaka 2017, Prof. Msanjila alisema hakuna changamoto katika utekelezaji wa sheria na kueleza kuwa serikali kupitia Wizara ya Madini inapokea wawekezaji wengi wenye utayari na nia ya kuwekeza nchini, huku utekelezaji wa sheria hiyo ukiwa si kikwazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako