• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China kufanyika tarehe 3 Machi Beijing

    (GMT+08:00) 2019-02-28 20:51:24

    Mkutano wa tano wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la awamu ya 13 la China umefunguliwa leo mjini Beijing.

    Kwa mujibu wa uamuzi uliowekwa kwenye mkutano huo, mkutano wa pili wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China utafanyika tarehe 3 Machi mwaka huu. Ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na kusikiliza na kukagua ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya baraza hilo, pamoja na ripoti kuhusu mapendekezo yaliyotolewa. Pia kuhudhuria mkutano wa pili wa Bunge la 13 la Umma la China na kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine, pia kujadili mswada wa sheria kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara wa nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako