• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la kiuchumi la Guangdong, Hongkong na Macao litajengwa kuwa kituo cha kimataifa cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia

    (GMT+08:00) 2019-03-01 20:26:05

    Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China hivi karibuni imeandaa mkutano na waandishi wa habari ikieleza hali kuhusu Mpango wa maendeleo kwenye eneo la kiuchumi la Guangdong, Hongkong na Macao. Ofisi hiyo imedokeza kuwa, katika siku za baadaye, eneo hilo litaonesha sifa ya sehemu hizo tatu, kujihusisha katika mtandao wa uvumbuzi wa dunia, na kujengwa kuwa kituo cha kimataifa chenye ushawishi duniani cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia.

    Kwa mujibu wa mpango huo, eneo la kiuchumi la Guangdong, Hongkong na Macao litajengwa kuwa eneo lenye uhai na ushindani mkubwa. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Luo Wen ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kimataifa cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ni kipaumbele cha ujenzi wa eneo hilo, na pia itaonesha sifa kubwa ya eneo hilo, anasema:

    "Ujenzi huo unalingana na mipango ya jumla ya serikali katika kufanya uvumbuzi wa kikanda, na kuharakisha hatua ya kupata ukuaji wa uchumi kupitia uvumbuzi."

    Hivi sasa katika ushirikiano kati ya Guangdong na Hongkong, maandalizi ya ujenzi wa eneo la ushirikiano wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia la Hongkong yamepata maendeleo mjini Shenzhen. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Hongkong kimejengwa mjini Guangzhou, na vyuo vikuu 6 vya Hongkong vimeanzisha mashirika 72 ya utafiti wa sayansi mjini Shenzhen. Naibu mkuu wa mkoa wa Guangdong Bw. Lin Shaochun anasema:

    "Fedha katika matumizi ya sayansi ya mkoa wa Guangdong pia zinaweza kutumiwa katika mikoa ya utawala maalumu ya Hongkong na Macao. Wakati huo huo mashirika ya utafiti wa sayansi na maabara mkoani Guangdong pia zitafunguliwa kwa Hongkong na Macao."

    Mkuu wa Idara ya mambo ya siasa kwenye serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bw. Zhang Jianzong ameeleza kuwa, katika siku za baadaye Hongkong itaingiza kampuni za kimataifa za uvumbuzi wa sayansi kwenye eneo hilo la kiuchumi. Mkurugenzi wa utafiti wa sera na maendeleo ya kikanda wa mamlaka ya utawala maalumu wa Macao Bw. Mi Jian pia ameeleza kuwa Macao itaimarisha ushirikiano na miji mingine kwenye eneo hilo.

    Katika kipindi kijacho, eneo la kiuchumi la Guangdong, Hongkong na Macao litavutia na kutumia vya kutosha maliasili ya uvumbuzi duniani, kuzisaidia kampuni, teknolojia na bidhaa kwenda katika dunia nzima, ili kuhimiza ufunguaji mlango na ushirikiano wa uwezo wa uvumbuzi katika eneo kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako