• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua mpango wa kuendeleza video ya Ultra HD

    (GMT+08:00) 2019-03-03 18:38:27

    Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China, Idara Kuu ya Radio na Televisheni ya Taifa ya China na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG High-Definition Alhamisi zilitoa "Mpango wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Viwanda vya Video ya Ultra High-Definition (HD) wa kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2022". Kwa mujibu wa mpango huo, China itaendeleza viwanda vyenye thamani ya Yuan trilioni 4 vinavyohusu video ya Ultra HD ikiwemo chip, panel, mawasiliano ya simu na huduma za kidijitali.

    Channel ya kwanza ya televisheni ya 4K Ultra HD duniani ilizinduliwa miaka minne iliyopita nchini Korea Kusini, na baadaye Marekani, Ulaya na Japan zikaanza kuzindua miradi ya maendeleo ya video ya Ultra HD. Kutokana na ushindani wa sokoni, gharama za kupata huduma za vipindi vya 4K zimepungua na kukubaliwa na watu wa kawaida.

    Takwimu zinaonyesha kuwa video itachukua asilimia 85 ya matumizi ya mitandao ya internet katika siku za baadaye, na asilimia 80 ya wateja watapenda kulipia huduma za video bora. Mwenyekiti wa zamu wa kampuni ya Huawei Xu Zhijun alitabiri kuwa ifikapo mwaka 2020, idadi ya watumiaji wa 4K nchini China itafikia milioni 200, na kuizidi idadi ya jumla nchini Marekani na Ulaya kwa pamoja, na China itakuwa soko kubwa zaidi la video ya 4K Ultra HD duniani.

    Tarehe mosi, Oktoba mwaka jana, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilizindua rasmi channel la 4K Ultra HD. Nyuma ya video hizo bora zilizotangazwa, kuna mlolongo wa kiviwanda na ubunifu wa teknolojia kutoka utengenezaji wa vipindi, uzalishaji wa mashine hadi uwezo wa mtandao wa internet na huduma za kidigitali. Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya China, thamani ya viwanda vinavyohusu video ya Ultra HD itafikia trilioni 4 nchini China ifikapo 2022.

    Nchini Japan, mpango wa kuhimiza video ya Ultra HD umetajwa na serikali kuwa ni sehemu ya Mkakati wa Ustawi wa Japan. Serikali ya Japan impeanga kuwa ifikapo mwaka 2025, televisheni ya 4K Ultra HD itamfikia kila mtu ifikapo 2025. Vilevile nchini Marekani, kampuni za mawasiliano ya simu zinashirikiana na kampuni za kutengeneza vipindi, ili kupanua maslahi ya kampuni na kukidhi mahitaji ya wateja kwa video za Ultra HD.

    Ikilinganishwa na Marekani na Japan, mlolongo wa viwanda vya video ya Ultra HD nchini China utapata soko kubwa. Kwa mujibu wa mpango wa utekelezaji wa maendeleo ya viwanda vya video ya Ultra HD, katika miaka mine ijayo, China itahimiza maendeleo ya teknolojia muhimu za kutengenezea video ya Ultra HD, na ifikapo mwaka 2022, China itatumia teknolojia ya video ya Ultra HD katika sekta sita ikiwemo radio na televisheni, burudani, ulinzi wa amani na kamera ya uchunguzi, huduma za matibabu, usimamizi bora wa usafiri barabarani na utengenezaji kiviwanda.

    Video ya Ultra HD inapatikana kwa usambazaji bora, na kutokana na ushindani mkali wa teknolojia ya mtandao wa 5G, China, Japan, Marekani na Korea Kusini zimepanga kufanya huduma za mtandao wa 5G ziwafikie watu wa kawaida mwaka 2020, hata mwaka 2019. Hii imehimiza kasi ya mipango ya washiriki wa viwanda vinavyohusu video ya Ultra HD duniani.

    Kwa mfano, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Alhamisi lilifanikisha utengenezaji wa pamoja wa video ya 4K Ultra HD. Miji 12 ya China ikiwemo Shanghai ilisambaza signal 16 za video ya 4K Ultra HD kwa kutumia mtandao wa 5G kwa maabara ya mtandao 5G ya CMG iliyopo makao makuu hapa mjini Beijing. Na picha hizo za Ultra HD zilisambazwa kwa mtandao wa 5G kwenye simu ya mkononi ya kisasa aina ya Foldable yenye uwezo wa 5G iliyozinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Huawei.

    "Mpango wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Viwanda vya Video ya Ultra High-Definition (HD) wa kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2022" utakaotekelezwa hatua kwa hatua itaonyesha kazi zake katika kuongeza matumizi ya ngazi ya kati na ya juu nchini China na kuinua kiwango cha maisha ya watu, kuimarisha msingi kuu wa viwanda vinavyohusu video ya Ultra HD, kuongeza idadi ya vipindi vya Ultra HD, kuinua uwezo wa usambazaji mtandaoni, na kufanya dunia iliyojaa video ya Ultra HD iwe karibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako