• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa CPPCC wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2019-03-03 19:05:54

    Kikiwa chombo cha ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC limefanya kazi muhimu katika shughuli za kisiasa nchini China. Leo alasiri, mkutano wa pili wa awamu ya 13 ya CPPCC umefunguliwa hapa Beijing, ambapo mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Wang Yang amesisitiza kuwa, huu ni mwaka muhimu katika kufanikisha kazi za kujenga jamii yenye maisha bora, na CPPCC ikiwa chombo maalumu cha kufanya mashauriano, inapaswa kuchangia mafanikio ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora na kufanya vizuri kazi za kuzuia kutokea kwa hatari kubwa, kupunguza umaskini kwa malengo sahihi na kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira, kuonesha nafasi za mashauriano ya kisiasa, uangalizi wa kidemokrasia, kushiriki na kujadili masuala ya kisiasa na kuinua ubora wa mapendekezo na kupanua maoni ya pamoja.

    Leo saa tisa alasiri, mkutano wa pili wa awamu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC umefunguliwa hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais Xi Jinping. Bw. Wang Yang ametoa ripoti ya kazi kwa niaba ya kamati ya kudumu ya CPPCC. Katika siku 11 zijazo za mkutano huo, wajumbe zaidi ya 2,100 wa CPPCC watajadili ripoti hiyo, na kutoa mapendekezo juu ya mageuzi na maendeleo ya China.

    Mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa kwanza kwa awamu ya 13 ya CPPCC kufanya majukumu yake, ikiwemo kusimamia kwa pande zote na kwa njia za kisayansi maswala mbalimbali yanayofuatiliwa na wajumbe wa CPPCC kutokana na vitendo vya kifedha vinavyokiuka kanuni, kuhimiza maendeleo ya soko la nyumba, hadi kuhimiza huduma za madaktari wa familia na kushughulikia betri zilizotupwa za magari yanayotumia nishati mpya bila kuchafua mazingira. Kuhusu kazi za mwaka mmoja uliopita, mwenyekiti wa CPPCC Bw. Wang Yang amesema awamu ya 13 ya CPPCC imefanya majukumu yake kwa ajili ya wananchi, kusaidia kuboresha maisha ya watu na maendeleo ya jamii. Anasema,

    "Ili kusaidia utekelezaji wa mkakati wa China yenye afya, CPPCC limefanya mashauriano juu ya kuboresha mfumo mpya wa uendeshaji wa hospitali za umma, kuimarisha huduma za matibabu na kuandaa madaktari wenye ujuzi mpana mashinani, kuboresha mfumo wa kuwatunza wazee, na kuhimiza ujenzi afya kwa wananchi wote. Pia limefuatilia ujenzi wa utawala wa sheria, na kutoa mapendekezo kuhusu utungaji wa kanuni za kuwalinda vijana kwenye mtandao wa internet, sheria ya kulinda maslahi wanajeshi wastaafu, kanuni za usajili wa mashirika ya kiraia na mageuzi ya uwajibikaji kisheria, na kusaidia kuimarisha utawala wa nchi kwa sheria."

    Kupanua njia za demokrasia kwa mashauriano ni moja ya kazi zinazofanywa na CPPCC katika miaka ya karibuni. Mwaka jana CPPCC ilizindua programu kwenye simu ya mkononi kwa wajumbe ili kufanya mashauriano kwenye mtandao wa internet. Naibu katibu mkuu wa mkutano wa pili wa awamu ya 13 ya CPPCC na msemaji Bw. Guo Weimin amesema hii ni kazi inayostahili kusifiwa kwa awamu hii ya CPPCC, na njia hii inayotumia mtandao wa internet na vyombo vipya vya habari, imeondoa vikwazo vya kijiografia na muda na kuongeza hisia za wajibu na ushiriki wa wajumbe. Anasema,

    "Mwaka jana CPPCC ilifanya majadiliano kwa njia hiyo mara mbili, safari moja tulijadili kuboresha mazingira ya kibiashara na kuhimiza maendeleo ya sekta binafsi, na safari nyingine tulijadili maendeleo mazuri ya sekta ya usambazaji vifurushi. Naweza kusema kujadili mambo ya kisiasa na kufanya mashauriano kwenye mtandao wa internet kuna ufanisi, kwani wajumbe wengi wanaweza kushiriki, kuwasiliana vizuri, na kujadili kwa kina."

    Mwaka huu ni mwaka wa 70 tangu CPPCC izinduliwe, pia ni mwaka muhimu kwa China kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora. Bw. Wang kwenye ripoti yake ya kazi amesema mwaka huu mpya, CPPCC itaangalia ujenzi wa jamii yenye maisha bora, kufanya vizuri kazi za kuzuia kutokea kwa hatari kubwa, kupunguza umaskini kwa malengo sahihi, na kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira, kuonesha nafasi za mashauriano ya kisiasa, uangalizi wa kidemokrasia, kushiriki na kujadili masuala ya kisiasa na kuinua ubora wa mapendekezo na kupanua maoni ya pamoja. Anasema,

    "(CPPCC) itafanya mikutano ya kamati ya kudumu kuhusu kuhimiza maendeleo mazuri ya uzalishaji kiviwanda na kufanya elimu iridhishe wananchi. Pia itafanya mashauriano kuhusu kuhimiza maendeleo yanayotokana na ubunifu na kuimarisha huduma za utamaduni wa umma wa kimsingi katika sehemu za vijijini. Pia itaangalia masuala ya kijamii kama vile kuhimiza ajira, na kulinda taarifa za watu binafsi."

    Ikiwa jukwaa muhimu la kuonesha demokrasia kwa njia ya mashauriano, mashauriano ya kisiasa ya CPPCC yanaangalia masuala yanayohusu siasa, uchumi, utamaduni na maisha ya jamii, na kabla ya kufanya maamuzi, kunakuwa na mashauriano. Bw. Wang Yang amesema CPPCC inasaidia kuboresha maisha ya watu, na kuwaongezea hisia za kupata, kufurahi na kuwa na usalama. Habari zinasema wajumbe wa awamu hii ya CPPCC wanatoka sekta 34, na asilimia 59.9 kati yao sio wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC. Bw. Wang anasema,

    "CPPCC imekamilisha mfumo wa kutoa maelezo, kufanya mazungumzo na kufanya utafiti wa pamoja, kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kufanya majukumu kwa wanachama wasio wa CPC, watu wa sekta za viwanda na biashara na watu wasio wanachama. Pia imepanua njia za mawasiliano na wasomi wasio wanachama wa CPC, wafanyabiashara wa sekta binafsi na watu wa tabaka jipya la kijamii."

    Mwaka jana, CPPCC ilitoa kipaumbele kwa kazi za kuinua ubora wa kazi, na kufanya kazi za CPPCC igeuke kutoka "kufanya kazi gani" au "kufanya kazi vipi" hadi "kupata ufanisi gani". Katika mwaka huu mpya, Bw. Wang ametoa maagizo mapya kuhusu kuinua ubora wa kazi za CPPCC. Bw. Wang anasema,

    "Ni lazima kufuatilia kwa karibu mada ya kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora, kuamua mahali pa kufanyia utafiti, na kuachana na vitendo vya kueleza kijuujuu, na wajumbe wanapaswa kutoa mapendekezo kwa mujibu wa utafiti na yanayotekelezeka"

    Bw. Wang Yang amesisitiza kuwa wajumbe wa CPPCC wanapaswa kutafiti hali halisi, kutoa mapendekezo yanayotekelezeka na kukusanya maoni ya pamoja, kuinua ubora wa mapendekezo na kukusanya maoni ya pamoja na kusaidia kazi za kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako