• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi kuu Tanzania Bara: Simba yazima kelele za Stand United yaibamiza 2-0

  (GMT+08:00) 2019-03-04 11:45:48

  Wekundu wa Msimbazi klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam inasema kituo kinachofuata ni Algeria, baada ya kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za viporo vya ligi kuu Tanzania bara.

  Simba wameifunga Stand United kwa mabao 2-0 uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco aliyefunga mabao yote mawili.

  Mechi nyingine za ligi hiyo, wakata miwa wa Turiani Mtibwa imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mbao FC, nayo Singida United imewashinda Wajelajela Tanzania Prisons 2-1, Kagera sugar imeisambaratisha Lipuli kwa mabao 2-0 huku Mbeya City wakilazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako