• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Umma la China wafanyika leo

    (GMT+08:00) 2019-03-04 12:26:14

    Mkutano wa maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Umma la China NPC umefanyika leo asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Spika wa Bunge la Umma la China Bw. Li Zhanshu ameendesha mkutano huo.

    Mkutano huo umechagua jopo la wenyekiti na katibu mkuu wa Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Umma la China.

    Kwa mujibu wa ajenda zilizopitishwa kwa kupigwa kura kwenye mkutano huo, Mkutano wa Pili la Bunge la 13 la Umma la China utapitia ripoti ya kazi ya serikali, hali ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii ya mwaka 2018, na ripoti kuhusu mswada wa mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii ya mwaka 2019, pia utapitia hali ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa ya mwaka 2018, ripoti ya kazi ya Halmashauri ya kudumu ya Bunge, ripoti ya kazi ya Mahakama kuu, na ripoti ya kazi ya Idara kuu ya uendeshaji mashitaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako