• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa Bunge la China asema China na Marekani zinapaswa kuimarisha mashauriano ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-03-04 13:05:55
    China na Marekani zinapaswa kuongeza mashauriano ya kiuchumi na kibiashara ili kufikia makubaliano yanayonufaisha pande zote mbili.
    Hayo yamesemwa na msemaji wa Mkutano wa pili wa Bunge la 13 la Umma la China Bw. Zhang Yesui, ambaye pia amesema timu za kiuchumi na kibiashara za nchi hizo mbili zimefanya mashauriano ya kina na yenye matunda, na kupata maendeleo muhimu katika masuala mengi yanayofuatiliwa kwa pamoja.
    Ameongeza kuwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani unanufaishana kimsingi, na China inatarajia kuendelea kufanya mashauriano na Marekani ili kufikia makubaliano yanayonufaisha pande zote mbili.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako