Matumizi ya China yenye ukomo katika mambo ya ulinzi yanayolenga kulinda mamlaka, usalama na ukamilifu wa ardhi hayatoi tishio lolote kwa nchi yoyote.
Hayo yamesemwa na msemaji wa Mkutano wa pili wa Bunge la 13 la Umma la China Bw. Zhang Yesui, ambaye ameongeza kuwa, kama nchi fulani ni tishio la kijeshi kwa nchi nyingine au la, kamwe haiamuliwi na ongezeko la matumizi yake katika mambo ya ulinzi, bali inaamuliwa na sera zake za mambo ya nje na ulinzi wa kitaifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |