• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa mashauriano ya kisiasa wachangia maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2019-03-04 19:02:38

    Mkutano wa Bunge la Umma la China na mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China hufanyika mwezi Machi kila mwaka. Hii ni mikutano miwili muhimu ya China katika kutunga mipango ya maendeleo ya kitaifa. Ukiwa mfumo wa kisiasa wenye umaalumu wa China, mfumo wa mashauriano ya kisiasa umechangia maendeleo ya China katika miaka 70 iliyopita.

    Mivutano ya kisiasa ni hali ya kawaida duniani, na hata katika baadhi ya nchi inatokea mara kwa mara. Kwa mfano hivi karibuni mvutano kati ya vyama viwili vya bunge la Marekani ulisababisha kusimamishwa kwa serikali, na kuleta athari kubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii na maisha ya watu.

    Wananchi wa China ambayo ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani wana matarajio tofauti kuhusu maslahi yao. Lakini wana tarajio moja la pamoja ambalo ni kutimiza ustawi wa taifa. Ukiwa mfumo muhimu wa majadiliano kati ya vyama mbalimbali, mfumo wa mashauriano ya kisiasa ni njia kuu ya China katika kuhimiza maoni ya pamoja na ushirikiano kati ya watu wa hali tofauti.

    Kauli mbiu ya mfumo wa mashauriano ya kisiasa wa China ni mshikamano na demokrasia. Kwa kuwa wajumbe wanaohudhuria mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa wanawakilisha maslahi ya watu wa hali mbalimbali, hivyo mfumo huo unaweza kuunganisha nguvu zote za kijamii. Kwa mfano asilimia 60.2 ya wajumbe wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisasa si wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China, na wanatoka vyama vingine, na mashirikisho ya kijamii, au ni watu wasio na chama cha kisiasa.

    Tangu mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, kamati kuu ya chama hicho imetaka Baraza la Mashauriano ya Kisiasa lizingatie mipango ya kitaifa ya maendeleo na masuala muhimu ya maisha ya watu, na kufanya usimamizi wa kidemokrasia kwa utawala. Wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa katika ngazi mbalimbali wana ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa kutoa maoni na mapendekezo kwa kazi za serikali katika ngazi mbalimbali.

    Huu ni mwaka wa 70 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, na pia ni mwaka wa 70 tangu mfumo wa mashauriano ya kisiasa wa China uanzishwe. Uzoefu wa miaka hiyo umethibitisha kuwa mfumo huo ni jukwaa muhimu la majadiliano ya kisiasa nchini China, na pia ni mfumo wa uzalendo wenye uwakilishi mpana, na umetoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

    Kuna njia tofauti katika kutekeleza demokrasia duniani. Mifumo ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa imetoa nguvu isiyoishika kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini China, na imekuwa njia nyingine nzuri ya kutekeleza demokrasia ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako