Mkutano wa pili wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China utaanza kesho saa 3 asubuhi katika Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing.
Katika mkutano huo, waziri mkuu wa China Li Keqiang anatarajiwa kuwasilisha ripoti ya kazi za serikali, kukagua utekelezaji wa mpango wa uchumi wa taifa na maendeleo ya jamii katika mwaka 2018, na miswada ya mpango wa uchumi wa taifa na maendeleo ya jamii katika mwaka 2019.
Pia mkutano huo utakagua hali ya utekelezaji wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa katika mwaka 2018 na miswada ya bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa katika mwaka 2019. Wawakilishi kutoka pande mbalimbali watafanya mkutano wa pamoja kesho alasiri kukagua na kujadiliana juu ya ripoti ya kazi ya serikali.
Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) litatangaza moja kwa moja ufunguzi wa mkutano huo na pia vyombo vikuu vya habari vya China vitatangaza mkutano huo kupitia tovuti na mitandao mbalimbali ya kijamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |