Msemaji wa wa Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Umma la China Bw. Zhang Yesui amesema, maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.
Bw. Zhang amesema miongoni mwa ajenda za mkutano huo, kupitisha mswada wa sheria ya uwekezaji kutoka nje kunafuatiliwa sana. Amesema lengo la kutunga sheria hiyo ni kufanya uvumbuzi kuhusu utaratibu wa kisheria wa uwekezaji huo ili kuendana na mahitaji ya kujenga mfumo mpya wa wazi wa uchumi.
Amesema, jumla ya nchi na mashirika ya kimataifa 152 zimesaini makubaliano ya ushirikiano na China kuhusu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na mwaka jana pekee, nchi 67 zimesaini nyaraka kama hizo na China.
Kuhusu suala la biashara kati ya China na Marekani, Bw. Zhang amesema, nchi hizo zinapaswa kuongeza mashauriano ya kiuchumi na kibiashara ili kufikia makubaliano yanayonufaisha pande zote mbili. Amesema, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo ni wa kunufaishana, na China inatarajia kuendelea kufanya mashauriano na Marekani ili kufikia makubaliano yanayonufaisha pande zote mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |