Rais Xi, ambaye pia katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Tume kuu ya Jeshi, alisema hayo wakati akijiunga kwenye mjadala wa jopo la pamoja uliohudhuriwa na washauri wa kisiasa kutoka sekta ya utamaduni sanaa, na sayansi ya kijamii. Washauri hao wako mjini Beijing kwa kikao cha kila mwaka cha Mkutano wa Ushauri wa Siasa wa Watu wa China (CPPCC).
Rais Xi kwanza aliwasikiliza wanachama wanane wa CPPCC ambao walizungumzia juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jukumu la majumba ya makumbusho, sanaa ya uvumbuzi na kujenga falsafa na sayansi za kijamii zenye sifa za Kichina.
"Wataalamu katika sekta za utamaduni, sanaa, falsafa na sayansi za kijamii ni wakuzaji muhimu wa jamii," Rais Xi alisema.
Aliwahimiza wataalamu katika sekta hizo kuzingatia mbinu zinazowanufaisha watu, kukaa karibu na watu na kutafakari maisha yao katika kazi zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |