• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China asisitiza kujiamini zaidi kiutamaduni

    (GMT+08:00) 2019-03-05 09:09:01

    Rais Xi Jinping wa China amewataka waandishi, wasanii na wananadharia kuimarisha moyo wa kujiamini kiutamaduni, kuwahudumia watu kwa kazi bora, na kuongoza umma kwa maadili ya kiwango cha juu.

    Rais Xi, ambaye pia ni Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya chama, alitoa kauli hiyo aliposhiriki kwenye mjadala wa wajumbe wanane kutoka sekta ya utamaduni, sanaa na sayansi ya kijamii, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa pili wa Baraza la awamu ya 13 ya mashauriano ya kisiasa CPPCC.

    Alipotoa hotuba baada ya kusikiliza maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe hao, Rais Xi amesema jukumu la wafanyakazi kwenye sekta ya utamaduni, fasihi, sanaa, falsafa na sayansi ya kijamii ni kurutubisha mzizi na roho ya taifa.

    Amesema ubora wa kazi za kiutamaduni, fasihi na sanaa umeendelea kuimarishwa, na maendeleo ya falsafa na sayansi ya kijamii yenye umaalumu wa kichina pia yameharakishwa. Rais Xi ametoa wito wa juhudi za kutekeleza jukumu la kuweka kumbukumbu za maandishi na kutukuza zama mpya.

    Akisisitiza kanuni ya kutoa kipaumbele kwa watu, rais Xi amesema watu ndio ni chanzo cha uvumbuzi, na kwamba wafanyakazi wa utamaduni, fasihi na sanaa wanapaswa kushiriki kiutendaji, kufuatilia kwa makini maisha ya watu, na kueleza matarajio ya umma.

    Rais Xi pia amewataka wafanyakazi wa falsafa na sayansi ya kijamii kufanya tafiti zaidi mashinani ili kujua hali halisi ya maisha ya wananchi.

    Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kutoa kazi bora kwa wananchi, akisema kazi zote zenye thamani za fasihi, sanaa na tafiti za kitaaluma zinatakiwa kuonesha uhalisi na kusaidia kutatua matatizo na changamoto halisi.

    Amesema watendaji wote wa sekta ya utamaduni, fasihi, sanaa, falsafa na sayansi ya kijamii wanabeba majukumu muhimu ya kuelimisha mawazo, kulea hisia na kufariji mioyo, na amewataka kuweka mfano kwa jamii kwa nia ya makuu, maadili mazuri na hisia za kifahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako