Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amesema katika ripoti yake ya kazi ya serikali ya China kuwa, China itaharakisha kujenga mfumo wa pamoja wa soko huria wa kisasa, ulio wazi na wa ushindani wenye utaratibu, na kuweka mazingira ya biashara ya kufuata sheria, kimataifa na kirahisi. Hivyo serikali ya China itapunguza zaidi orodha ya sekta za kuzuiliwa kuingia kwenye soko, kuhimiza utekelezaji wa kanuni ya kutoa ruhusa ya kuendesha biashara kwa kufuata sheria, kupunguza kwa kiasi kikubwa mgawanyo wa rasilimali wa moja kwa moja, kupunguza mlolongo wa shughuli za idhini kadiri iwezekanavyo, kuhimiza ushindani wenye usawa kwa kufuata usimamizi wa haki, na kuharakisha kuondoa kanuni na vitendo husika vinavyozuia umoja wa soko na ushindani wenye usawa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |