• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatangaza mikakati ya mambo ya utawala ya mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-03-05 13:54:23

  Mkutano wa mwaka wa Bung la Umma la China ambalo ni chombo cha ngazi ya juu cha kutunga sheria cha China umefunguliwa leo asubuhi mjini Beijing, ambapo waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali ya mwaka uliopita na mikakati ya mambo ya utawala ya nchi ya mwaka huu.

  Katika mwaka 2018 ambao ulikuwa ni mwaka wa kwanza kwa serikali ya awamu mpya kutekeleza majukumu yake, licha ya kukabiliwa na changamoto za ndani na nje ya nchi, China ilitimiza malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka 2018, uchumi uliendelea kwa kasi katika hali inayofaa , miundo ya uchumi iliboreshwa siku hadi siku, nafasi ya mazingira ya biashara ilipanda juu zaidi katika orodha ya dunia, na ufunguaji mlango ulipanuliwa zaidi.

  Bw. Li Keqiang amesema mwaka huu uchumi wa China utakabiliwa na shinikizo kubwa la kushuka, kitu ambacho kimeonyesha hali isiyo ya kuridhisha ya uchumi wa China, kama vile kupungua kwa kasi ya ongezeko la matumizi, pengo kati ya mazingira ya biashara na matarajio ya wafanyabiashara, na ukosefu wa nguvu za ubunifu wa kujitegemea na teknolojia muhimu. Akisema,

  "Wakati uchumi wa China unakabiliwa na hatari ya kushuka, ni lazima kushughulikia vizuri uhusiano kati ya serikali na soko, na kutegemea mageuzi na kufungua mlango kwa kuhamasisha nguvu za uhai za makampuni na wafanyabiashara. Iwapo makampuni na wafanyabiashara wana hamasa , wanaweza kujipatia nguvu za kujiendeleza na kuzuia uchumi ushuke zaidi. Ni lazima kuhimiza mageuzi na kufungua lango, kuongeza kasi ya kujenga mfumo wa soko la kisasa unaofungua mlango na wenye ushindani wa kufuata utaratibu, kulegeza masharti ya kuingia kwenye soko, kuimarisha usimamizi wa haki, kuandaa mazingira ya biashara inayotawaliwa kwa sheria, ya kimataifa, na yenye urahisi, na kufanya makampuni na wafanyabiashara kuwa na uchangamfu zaidi."

  Ripoti hiyo ya kazi ya serikali pia imeweka lengo kuu linalotarajiwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya China kwa mwaka huu, yaani ongzeko la pato la taifa GDP kwa mwaka huu kuwa kati ya 6% na 6.5%.

  Ripoti hiyo imeeleza kuwa China inatakiwa kushika vizuri sera za jumla, kuendelea kutekeleza sera zenye juhudi na za hatua madhubuti kuhusu mambo ya fedha, kutoa kipaumbele kwa soko la ajira, kuimarisha uratibu na ushirikiano wa sera mbalimbali, na kuhakikisha uchumi unaendelea katika kiwango kinachofaa na jamii inaendelea vizuri. Bw. Li Keqiang akifafanua anasema,

  "Mwaka huu, nakisi ya bajeti itadhibitiwa ndani ya 2.8%, ambayo ni juu zaidi kuhusu bajeti ya 0.2% la mwaka jana. Uamuzi wa kuongeza naski ya bajeti umefanywa baada ya kufikiria mapato na matumizi ya fedha na utoaji wa dhamama maalumu, na pia kubakiza nafasi za matumizi ya sera kama hatari zinatokea katika siku za baadaye."

  Mwaka jana, China iliadhimisha miaka 40 ya mageuzi na kufungua mlango, na kuonesha nia thabiti na imani ya kufungua zaidi mlango kwa dunia. Katika mwaka huu mpya wakati China inapoanza raundi mpya ya mageuzi na kufungua mlango, utadawazi na ushirikiano wa kimataifa vinakabiliwa na changamoto kubwa. Ripoti inasema China itafungua mlango kwenye kiwango cha juu ili kuhimiza mageuzi yaendelezwe kwa kina na kwa pande zote. Anasema,

  "China itaongeza nguvu ya kuvutia uwekezaji kutoka nje. China italegeza udhibiti wa kuingia sokoni, kupunguza sehemu za kuzuiliwa kwa uwekezaji wa nje, na kuyaruhusu mashirika binafsi ya nje kufanya biashara kwenye sekta nyingi zaidi. Zaidi ya hayo China itaimarisha juhudi za kulinda haki na maslahi halali ya wawekezaji kutoka nchi za nje. Mazingira ya uwekezaji ya China hakika yatakuwa bora zaidi, na fursa za maendeleo ya kampuni mbalimbali zitakuwa nyingi zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako