• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupiga kura kupitisha mswada wa sheria ya uwekezaji kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-03-05 18:50:01
    Bunge la Umma la China linatarajiwa kupiga kura wiki ijayo kupitisha muswada unaosubiriwa kwa hamu ambao una mabadiliko makubwa kwa wawekezaji wageni.

    Muswada huo wa sheria ya uwekezaji kutoka nje, utakuwa ni kitu kinachofuatiliwa katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la China ambacho kitafanyika kwa wiki mbili kuanzia kesho.

    Sheria hiyo inalenga kushughulikia malalamiko ya muda mrefu ya kampuni za nje.

    Muswada huo ukipitishwa, utaondoa masharti yanayotaka kampuni za nje kuhamishia China umiliki wa kiteknolojia wa siri za ushindani wa kibiashara wakati zinapotaka kuingia katika ubia na kampuni za China.

    Pia inaahidi kuondoa urefu wa mchakato kwa kampuni za kigeni kuingia soko la China. Mabadiliko hayo yatahakikisha kuwa wawekezaji kutoka nje watapata upendeleo sawa na kampuni za China katika sekta zote, isipokuwa zile nyeti zilizoanishwa katika "orodha hasi".

    China hutumia "orodha hasi" kuanisha maeneo ambayo hayatakiwi kuguswa na kampuni ambazo si za serikali au ambayo yanahitaji kampuni hizo kupitisha mchakato wa maombi na kusubiri yapitishwe.Hii inamaanisha kuwa kampuni za China na za nje zitahudumiwa bila ubaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako