Mkuu wa idara kuu ya ushuru wa forodha ya China Bw. Ni Yuefeng leo amesema, China itaendelea kupambana na biashara ya magendo ya takataka zinazotoka nchi za nje.
Bw. Ni amesema, China siku zote inapambana na biashara hiyo kwa nia thabiti, na imeimarisha usimamizi kwa maagizo ya takataka zinazoweza kurudia kutumika. Ameongeza kuwa mwaka huu China itafanya operesheni maalumu za kudhibiti biashara hiyo haramu.
Bw. Ni amesema, hivi sasa China inafanya ukaguzi mkali zaidi kwa takataka zinazoagizwa kutoka nchi za nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |