• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza dhamira ya kimkakati ya kuimarisha ujenzi wa ustaarabu wa kulinda mazingira ya asili

    (GMT+08:00) 2019-03-06 08:58:47

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza juhudi za kudumisha dhamira ya kimkakati ya kuimarisha ujenzi wa ustaarabu wa kulinda mazingira ya asili, haswa kwenye maeneo ya mpaka wa kaskazini.

    Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya Chama, amesema hayo alipohudhuria mjadala wa wajumbe kutoka mkoa wa Mongolia ya Ndani kwenye Mkutano wa pili wa Bunge la awamu ya 13 ya umma la China unaofanyika hapa Beijing.

    Rais Xi ametoa wito wa kuimarisha juhudi za kuhifadhi mfumo wa mazingira ya asili, akiwahamasisha wananchi kupambana kithabiti na uchafuzi wa mazingira. Amezitaka idara zote za serikali na serikali za mitaa zitekeleze kwa makini mipango ya Chama kwa ajili ya kujenga ustaarabu wa kulinda mazingira ya asili.

    Rais Xi amesema, kuujenga mkoa wa Mongolia ya Ndani kuwa ngao muhimu ya kulinda usalama wa kiikolojia kwenye sehemu ya kaskazini mwa China, ni kipaumbele cha kimkakati kilichotolewa kwa kuzingatia mahitaji ya maendeleo ya nchi nzima, na pia ni wajibu muhimu wa mkoa huo.

    Rais Xi ameainisha kuwa uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi vinafungamana kwa karibu na vinasaidiana. Katika mchakato wa China kubadilisha mkakati wake wa kukuza uchumi kutoka kutafuta kasi ya ukuaji, hadi kwenye kuzingatia ubora wa maendeleo, udhibiti wa uchafuzi na usimamizi wa mazingira ni majukumu mawili muhimu yanayotakiwa kufanikishwa.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa China inapaswa kutafuta mbinu mpya ya kutimiza maendeleo ya ubora wa juu, ambayo yanatoa kipaumbele kwa uhifadhi wa ikolojia na maendeleo yasiyoharibu mazingira.

    Amesema mkoa wa Mongolia ya Ndani wenye uanuwai wa mazingira ya asili yanayojumuisha misitu, mbuga, ardhi oevu, mito, maziwa na majangwa, una mfumo kamili wa kiikolojia ulioundwa kwa miaka mingi. Hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kuhuisha na kuhifadhi mazingira katika mkoa huo. Rais Xi ameagiza mapambano yenye dhamira na ufanisi, ya kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, akisema masuala ya kimazingira yanayofuatiliwa kwa karibu na wananchi ni lazima yatatuliwe kwa hatua mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako