• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi awataka viongozi wa mkoa wa Mongolia kuendelea kulinda mazingira

    (GMT+08:00) 2019-03-06 09:24:12

    Rais wa China Xi Jinping ametoa wito kwa manaibu wa Kongamano la Taifa la Watu kutoka Mkoa unaojiendesha wa Mongolia kuwa na mkakati wa kujenga uchumi usioathiri mazingira.

    Rais Xi alikutana na manaibu kutoka Mkoa wa Mongolia wakati wa mjadala wa jopo la Jumanne, siku ya kwanza ya kikao cha kila mwaka cha bunge China mjini Beijing.

    Alisema kuwa ulindaji wa mazingira nchini umejumuishwa kwenye mkakati wa jumla wa maendeleo nchini China, na kuelezea umuhimu wake katika maendeleo ya Mongolia.

    "Kuhakikishia maendeleo ya kijani" ni msemo ulitokea mara kwa mara wakati wa mjadala wa jopo la Jumanne.

    Rais Xi alisisitiza umuhimu wa kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira huku uchumi wa nchi ukibadilika kutoka ukuaji wa kasi na badala yake kuzingatia maendeleo ya ubora wa juu. Kwa hali yoyote mazingira hayawezi kutumika vibaya kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, alisema.

    Mkoa wa Mongolia ya ndani una makabila 55, na ilikuwa eneo la kwanza la linalojiendesha katika historia ya Jamhuri ya Watu wa China. Rais Xi alisema kuwa eneo hilo ni muhimu kwa kuhakikisha ulinzi wa mazingira katika maeneo makubwa ya kaskazini mwa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako