• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu bingwa Ulaya, hatua ya 16 bora-Madrid yafungasha virago

  (GMT+08:00) 2019-03-06 10:19:51

  Mechi za mzunguko wa pili, hatua ya 16 bora kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya, maarufu UEFA zimepigwa jana usiku huku timu nne zitajitupa uwanjani usiku wa leo.

  Borussia Dortmund ya Ujerumani, ilikuwa na kibarua dhidi ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza, na matokeo ni kuwa, Tottenham imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Dortmund.

  Mechi ya mzunguko wa kwanza, wawakilishi hao wa Ujerumani, walifungwa mabao 3-0 ugenini.

  Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Real Madrid ya Uhispania iliyokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Bernabeu na kukubali kipigo cha maana toka kwa Ajax ya Uholanzi kwa magoli 4-1.

  Usiku wa kuamkia kesho kutakuwa na michezo minne itakayopigwa baina ya FC Porto itakapovaana na AC Roma, nayo Paris Saint Germain itaumana na Manchester United.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako