• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Abiria watatizika kufuatia mgomo wa wafanyakazi katika uwanja wa JKIA

    (GMT+08:00) 2019-03-06 19:58:26
    Wasafiri wa ndege jumatano waliamkia kutatizika katika Uwanja wa Kimataifa wa JKIA mjini Nairobi kufuatia mgomo wa Wafanyakazi wa Usafiri wa Angani (KAWU) wakipinga mpango wa Shirika la Ndege la KQ kusimamia shughuli za uwanja wa JKIA.

    Mgomo huo wa wafanyakazi na wanachama wa Usafiri wa Angani (KAWU) umetatiza hali ya kawaida katika uwanja huo na kuathiri shughuli huku abiria wakikosa usafiri.

    Abiria walioathirika waliweka jumbe za kulalamika katika mitandao ya kijamii huku Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya ikitoa hakikisho kuwa hali ya kawaida itarejea.

    Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege (KAA) jumatano asubuhi,abiria walishauriwa kuwasiliana na mashirika ya ndege ambayo walipanga kutumia kupata habari kuhusu mipango yao ya safari.

    Kufikia sasa shughuli zimerejea hali ya kawaida katika uwanja huo wa kimataifa wa JKIA.

    Waziri wa Kilimo nchini Tanzania ,Japhet Hasunga,amesema uimarishaji wa mitandao ya usambazaji mbegu na viatilifu ni muhimu katika kuhakikisha tija inaongezeka kwenye uzalishaji mazao nchini humo.

    Hasunga aliyasema hayo jana wakati akizindua Mpango wa kuimarisha Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu ,unaotekelezwa na mradi wa nafaka na kampuni ya Kimataifa ya Corteva katika mikoa ya nyanda za juu Kusini.

    Alisema wakulima nchini Tanzania wanategemea sekta ya kilimo kuchangia katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia 65 ya wananchi na ina uwezo wa kutoa malighafi ya viwanda kwa asilimia 66 pamoja na kuchangia asilimia 100 ya chakula kinachopataikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako