• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa hatua nyingi zaidi ya kufungua mlango ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji kutoka nje

  (GMT+08:00) 2019-03-06 20:08:00

  Maofisa husika wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo hapa Beijing wamesema, mwaka huu uchumi wa China utaendelea kudumisha mwelekeo mzuri. Aidha, China itaendelea kupunguza orodha ya sekta zisizoruhusu uwekezaji kutoka nje, kupanua maeneo yanayokaribisha uwekezaji kutoka nje, kutoa kundi la tatu la miradi mikubwa ya uwekezaji kutoka nje, ili kuweka mazingira mazuri ya kibiashara kwa ajili ya uwekezaji kutoka nje.

  Ripoti ya kazi ya serikali imeeleza malengo makubwa ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China, ambayo yanaonyesha matakwa ya kuhimiza maendeleo yenye sifa bora, yanaendana na hali halisi ya China, na kuunganisha na lengo la kujenga jamii yenye maisha bora. Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. He Lifeng akizungumzia maendeleo ya uchumi wa China kwa mwaka huu, amesema,

  "tunaamini kwamba uchumi wa China utaendelea kudumisha utulivu na mwelekeo mzuri, kutimiza lengo la mwaka huu lililowekwa."

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari, naibu mkurugenzi wa kamati hiyo Bw. Ning Jizhe amesema, China itaendelea kuendeleza uchumi wa kufungua mlango kwa ngazi ya juu zaidi, kutekeleza utaratibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoka nje watendewe kama wa ndani na utaratibu wa usimamizi wa orodha ya sekta zisizoruhusu uwekezaji kutoka nje, kupanua maeneo yanayokaribisha uwekezaji kutoka nje ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya kibiashara.

  "kwanza ni kupunguza orodha ya sekta zisizoruhusu uwekezaji kutoka nje. Kutoa hatua za kufungua mlango zaidi katika sekta za kilimo, uchimbaji madini, utengenezaji na huduma, kuruhusu wafanyabiashara kutoka nje kuwekeza makampuni binafsi katika sekta nyingi zaidi. Mwaka huu China itaendelea kupunguza orodha ya sekta zisizoruhusu uwekezaji kutoka nje, na kuendelea kufanya majaribio ya kupanua kufungua mlango katika maeneo ya jaribio la biashara huria. Pili ni kupanua maeneo yanayokaribisha uwekezaji kutoka nje. Mwaka huu China itatangaza orodha ya sekta zinazokaribisha uwekezaji kutoka nje, kutoa sera yenye manufaa ya kutotoza ushuru wa vifaa kutoka nje na matumizi ya ardhi katika miradi yanayokaribisha uwekezaji kutoka nje. Tatu ni kuwawezesha wafanyabiashara kutoka nje watendewe kama wa ndani kabla na baada ya kuwaruhusu kuingia."

  Habari nyingine zinasema mkutano wa pili wa bunge la 13 la umma la China utapitisha mswada wa sheria ya uwekezaji kutoka nje. Bw. Ning amesema, sheria hiyo hakika itatoa uhakikisho wa kisheria wenye nguvu zaidi kwa maslahi ya wafanyabiashara kutoka nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako