Leo Tarehe 8 Machi kwenye Mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la umma la taifa la China, Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipojibu swali kuhusu hali ya Peninsula ya Korea, amesema mkutano wa Hanoi kati ya viongozi wa Korea ya kaskazini na Marekani uliomalizika hivi karibuni, ni hatua kubwa katika mchakato wa kutatua kisiasa suala la nyuklia la Peninsula. Pande hizi mbili zitaweza kuondoa vizuizi na kufanya mkutano tena, ili kubadilishana maoni kwa udhati ana kwa ana, hali hii yenyewe ni maendeleo ya kuhimiza hamasa, ambayo inastahiki kusifiwa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuzitia moyo pande mbili za Korea ya kaskazini na Marekani zidumishe uvumilivu na kuendelea kupiga hatua kufuata mwelekeo sahihi wa kuhimiza juhudi za kuifanya peninsula iwe sehemu isiyo na nyuklia, na kuanzisha utaratibu wa amani wa peninsula hiyo.
Bw. Wang Yi amesema, kama maendeleo kati yao yataendelea bila kusita na mwelekeo hautabadilika, lengo la kuifanya peninsula iwe sehemu isiyo na nyuklia hakika hatimaye litatimizwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |