Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo amesema kwenye Mkutano na waandishi wa habari kuwa, mwaka wa maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi wa China na Marekani ni mwaka muhimu kwa pande hizi mbili kufanya majumuisho kuhusu mambo yaliyopita na kupanga mambo ya baadaye. Njia ya siku za baadaye imeonekana wazi, yaani kuhimiza kwa pamoja kuendeleza uhusiano kati ya China na Marekani ulio wa uratibu, ushirikiano na utulivu. Hayo ni maoni muhimu ya pamoja waliyofikia marais wa nchi mbili China na Marekani, ambayo yangekuwa mwelekeo wa juhudi za pamoja za watu wa sekta mbalimbali za nchi hizi mbili.
Bw. Wang Yi alipojibu swali la mwandishi wa habari kuhusu Kampuni ya Huawei kutoa mashitaka dhidi ya serikalli ya Marekani alisema, vitendo vya hivi karibuni vilivyofanywa dhidi ya kampuni maalumu ya China na mtu binafsi, kimsingi siyo kesi ya kisheria tu, bali ni shinikizo la kisiasa lililotolewa kwa makusudi. Serikali ya China inaunga mkono kampuni husika na mtu binafsi kutumia silaha ya kisheria kwa kulinda haki na maslahi yao na wasinyamaze.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |