• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi asema, China na Afrika zitajenga jumuiya ya mustakabali wa pamoja yenye uhusiano wa karibu zaidi

    (GMT+08:00) 2019-03-08 11:44:28

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo amesema, urafiki kati ya China na Afrika ulianzia tangu Enzi na Dahari. Pande hizi mbili siku zote ni ndugu wazuri wa kushirikiana kutokana na mustakabali wao wa pamoja na katika hali ya dhiki na faraja. Hivi sasa uhusiano kati ya China na Afrika uko katika kipindi kizuri zaidi cha kihisotira, ushirikiano wa kunufaishana wa pande hizi mbili utaendelea kwenye safu ya mbele ya ushirikiano kati ya nchi za kimataifa na Bara la Afrika.

    Ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio zaidi, hivyo unalaumiwa na kupakwa matope. Lakini pande mbili China na Afrika zinaaminiana kwa kiwango cha juu, urafiki wa China na Afrika ulipitia majaribio mengi, na matunda ya ushirikiano kati ya pande mbili pia yametapakaa barani Afrika. Tumeona kuwa, viongozi wengi wa nchi za Afrika na watu wenye busara wa hali mbalimbali wamelaani hoja zile za ati "Mtego wa madeni" na "ukoloni mambo leo". Hayo yameonesha vya kutosha kuwa, maneno yoyote yasiyo na msingi hayana soko barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako