• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China afafanua mawazo ya kidiplomasia ya China

    (GMT+08:00) 2019-03-08 20:03:25

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye pia ni mjumbe wa taifa la China leo amekutana na waandishi wa habari, na kufafanua mawazo ya kidiplomasia ya China kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa.

    Amesema, Rais Xi Jinping wa China aliwahi kusema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita. Nchi maskini zinahitaji misaada ya jumuiya ya kimataifa ili kupata maendeleo zaidi, lakini baadhi ya nchi zilizoendelea zinapinga utandawazi wa uchumi, na kuyachukulia maendeleo ya nchi maskini kama ni chanzo cha changamoto zao za kiuchumi.

    Katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imepunguza idadi ya watu maskini nchini humo kwa milioni 800, na kuwa nchi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi.

    Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lilitolewa mwaka 2013 na rais Xi kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya pamoja duniani. Hadi sasa jumla ya nchi 123 na mashirika 29 ya kimataifa zimesaini makubaliano na China kuhusu pendekezo hilo. Bw. Wang amesema, pendekezo hilo si "mtego wa madeni" na "hila ya kisiasa", bali ni "mkate wa kunufaisha watu" na fursa ya kupata maendeleo ya pamoja.

    Lakini amesema kuna baadhi ya watu wana uhasama mkubwa na wanapenda kupaka matope maendeleo ya China. Hata baadhi yao wanadai "kutengana na China", na kuzitisha nchi nyingine kutokuwa karibu na China. Bw. Wang amesema, kutengana na China ni kama kutengana na fursa na mustakabali mzuri, na pia ni kutengana na dunia nzima.

    Aidha Bw. Wang Yi amehamasisha makampuni ya China yanayokandamizwa na baadhi ya nchi kujilinda kisheria, na kutokuwa "kondoo wanaosubiri kuchinjwa", kwani kujipatia maendeleo ni haki halali ya makampuni na mataifa yote.

    Amesema China inaaminiwa na nchi nyingi kutokana na njia yake ya amani ya kujiendeleza. Takwimu zilizotolewa na mashirika ya Ujerumani na Marekani zinaonesha kuwa, watu wa Ulaya wanaona kuwa China ni nchi inayoaminika zaidi kuliko Marekani.

    Methali ya kichina inasema, "Mtu maskini anajilea, na mtu tajiri anapaswa kunufaisha wengine". China inaaminiwa kuwa itatoa mchango zaidi kwa ajili ya amani ya dunia na maendeleo ya binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako