• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ni lazima kukamilisha mfumo wa huduma kwa ajili ya watoto, wanawake na wazee vijijini

    (GMT+08:00) 2019-03-08 21:15:17

    Rais Xi Jinping wa China amesema, ili kutimiza ustawi wa vijijini ni lazima kuboresha mfumo wa huduma kwa ajili ya watoto, wanawake na wazee vijijini.

    Rais Xi amesema hayo alipokutana na wajumbe kutoka mkoa wa Henan wanaohudhuria mkutano wa bunge la umma la China. Amesema kutokana na maendeleo ya uchumi ya kasi, watu wengi wa vijijini wamekwenda mijini kufanya kazi, masuala ya elimu ya watoto, utunzaji wa wazee na masuala mengine ya kijamii yameongezeka. Katika miaka ya hivi karibuni, China imezitaka serikali za mitaa kujenga mfumo kamili wa huduma kwa ajili ya watoto, wanawake na wazee vijijini.

    Rais Xi pia amesisitiza kuwa, ili kutimiza ustawi wa vijijini, pia inatakiwa kukamilisha utaratibu wa bima za pesheni, bima za matibabu na bima za matibabu ya magonjwa makubwa kwa watu wa mijini na vijijini, na kukamilisha utaratibu wa uhakikisho wa maisha ya kimsingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako