Siku chache zilizopita, Kampuni ya Airbus imetangaza kuwa, itatumia rasmi kituo chake cha kufanya uvumbuzi kilichoko Shenzhen, China ambacho ni kituo pekee kilichoanzishwa nayo barani Asia, ambapo itawatumia wataalamu wanyeji, teknolojia na nguvu bora za wenzi wa ushirikiano, ili kuogeza zaidi uwezo mpya wa Kampuni ya Airbus, na kujenga siku za baadaye za usafiri wa ndege.
Hatua hii ya Kampuni ya Airbus ni tafsiri yenye umuhimu mkubwa kuhusu China kufungua mlango kwa duru mpya kwenye kiwango cha juu. Katika hali ya mwaka jana ambayo uwekezaji kutoka nje wa kimataifa ulipungua kwa 19% katika dunia nzima, lakini uwekezaji vitega uchumi kutoka nje nchini China uliongezeka kwa 3%, mwelekeo huu umepelekea hali kwenye mwaka 2019. Takwimu mpya zilizotolewa na Wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, Mwezi Januari mwaka huu utumiaji halisi wa China wa vitega uchumi kutoka nje uliongezeka kwa 4.8%, ambapo uwekezaji wa vitega uchumi kutoka Marekani na Uholanzi uliongezeka kwa 124% na 95.6% mtawalia.
Hivi sasa nguvu na uwezo wa ufufukaji wa uchumi wa dunia nzima vinapungua, lakini China haijaacha hata kwa dakika moja kufungua mlango kwa duru mpya kwenye kiwango cha juu ili kutimiza maendeleo ya China ya sifa ya juu. Hatua moja dhahiri ni kuwa wajumbe wa Bunge la umma la China wapatao zaidi ya 2900 wako katika kuthibitisha Mswada wa Sheria kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara kutoka nje kwenye mkutano unaofanyika hapa Beijing, ambapo China inalenga kupitia sheria hiyo kwa kuhimiza uwekezaji wa wafanyabiashara kutoka nje, kulinda haki na maslahi yao halali, na kujenga mazingira ya biashara yaliyo ya usimamizi wa kisheria, ya kimataifa na yenye urahisi, ili kusaidia duru mpya ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu.
Kiongozi mkuu wa China Xi Jinping anaona kuwa, mafanikio ya uchumi wa China ya miaka 40 iliyopita yalipatikana katika hali ya kufungua mlango, uchumi wa China wa siku za baadaye utaendelea katika kipindi cha ukuaji wa sifa ya juu kutoka kipindi cha ongezeko la kasi, hivyo pia ni lazima uendelezwe kwenye hali ya kufungua mlango.
Wachambuzi wamedhihrisha kuwa, nia ya kutunga Sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara kutoka nje ni kuthibitisha utaratibu wa kimsingi na kanuni kuhusu kibali cha kuingiza, kuhimiza, kulinda na kusimamia uwekezaji wa wafanyabishara kutoka nje. Katika siku za baadaye matatizo watakayokabiliwa wafanyabiashara kutoka nje nchini China yataweza kushughulikiwa kwa haki, usawa na wazi kwa mujibu wa sheria hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |