Bw. Grandi ambaye yuko ziarani huko Beirut nchini Lebanon amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa UNHCR, wakimbizi wengi wa Syria nchini Lebanon wanapenda kurudi nyumbani kwao, ingawa wana wasiwasi juu ya masuala ya usalama wa Syria, makazi, na mahitaji ya kimsingi ya maisha, pamoja na masuala mengine ya kisheria.
Hata hivyo Bw. Grandi amesema kuwa UNHCR inashirikiana na serikali ya Syria kutatua masuala hayo.
Kutokana na makadirio ya serikali ya Lebanon, Wasyria wapatao milioni 1.5 walikimbia Lebanon toka msukosuko wa Syria kulipuka waka 2011.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |