• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mswada wa Sheria ya Uwekezaji kutoka Nje waonyesha dhamira na imani ya China ya kufungua zaidi mlango

    (GMT+08:00) 2019-03-10 18:37:53
    Mwenyekiti wa Shirika la wafanyabiashara la China Bw Li Jianhong jana alisema kuwasilisha mswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Wafanyabiashara kutoka nje kwenye Bunge la Umma la China kumeonyesha dhamira na imani ya China ya kufungua zaidi mlango, pia kutasaidia kuboresha mfumo na uwezo wa kiutawala nchini China.

    Bw. Li ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la taifa na sasa yupo Beijing kuhudhuria kikao cha mwaka cha baraza hilo, amesema sheria tatu zilizopo kuhusu mitaji kutoka nje zinatilia mkazo kuhamasisha kuvutia uwekezaji kutoka nje, lakini mswada huu wa sheria ya uwekezaji kutoka nje unatilia maanani ufunguaji mlango juu ya mambo ya kimfumo, ili kuhimiza wafanyabiashara kutoka nje wawekeze nchini China. Aidha, mswada huu utaweza kusaidia uchumi wa China upate maendeleo yenye ubora zaidi.

    Ameongeza kuwa mbali na kuvutia uwekezaji kutoka nje, China pia inapaswa kuongeza kasi ya kuwekeza nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako