• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abiria na wahudumu wote waliokuwemo katika ndege iliyoanguka ya shirika la Ethiopia wafariki dunia

    (GMT+08:00) 2019-03-11 06:42:57

     

    Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 MAX 8, iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kuelekea Nairobi ilianguka jana asubuhi na kuwaua abiria na wahudumu wote waliokuwemo. Kufuatia ajali hiyo iliyotokea dakika sita baada ya ndege hiyo kupaa, kampuni ya kutengeneza ndege hizo, Boeing inatarajiwa kutuma mafundi wake wa mitambo kwenye eneo la ajali hiyo kubaini ni kipi haswa huenda kilichangia ndege hiyo kuanguka.

    Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Bole uliopo jijini Adis Ababa. Ndege hiyo ilitoka katika uwanja wa ndege wa Bole 8:38Am na kupoteza mawasiliano dakika sita baadaye. Ndege hiyo ilikuwa imeratibiwa kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa JKIA saa nne unusu, saa za Afrika Mashariki.

    Akitoa ripoti kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines Tewolde Gebremariam amesema kuwa miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na :

    Wakenya 32, raia wa Canada 18, raia tisa wa Ethiopia , waitaliano wanane , Wachina wanane, wamarekani wanane , waingereza saba , Wafaransa saba , Wamisri sita, Wajerumani watano , Wahindi wanne na wanne kutoka Slovakia.

    Waastralia watatu, Waswis watatu, Warusi watatu , raia watatu kutoka Russia, s, Wakomoro wawili, Wahispania wawili, Wapoland wawili, Waisraeli wawili.

    Kulikuwa pia abiria mmoja mmoja kutoka nchi za ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, Togo, Msumbiji, Rwanda, Sudan, Uganda na Yemen.

    Katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa JKIA, ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wamefika kuwapokea wapendwa wao walijawa na huzuni wasijue cha kufanya.

    Nilikuwa nimekuja kumpokea shimeji yangu. Anaitwa Derrick Lugi. Alipaswa kuwasili saa nne na robo za asubuhi. Tulikuwa hapa kabla ya saa nne. Tulipoangalia kwenye kiwambo cha runinga ya matangazo ya usafiri wa ndege, ilisemekana kwamba ndege hiyo ilitua saa nne na robo. Lakini mwendo wa saa tano za mchana, tukaanza kusoma taarifa za kuhuzunisha kwenye mitandao kuhusu ajali ya ndege ya Ethiopian Airline, ambayo ilitoka Ethiopia muda ambao shemeji yangu alikuwa ameabiri.

    Waziri wa Uchukuzi James Macharia ambaye amekuwa kwenye uwanja wa ndge wa JKIA kufuatilia habari hii, alisema kwamba wanashirikiana na kwa karibu na shirika la ndege la Ethiopia wakati huu mgumu.

    Nimemtuma katibu wangu mkuu katika wizara ya Uchukuzi Esther Koimett pamoja na mkurugenzi mkuu wa usafiri wa ndege Bwana Nicholas Bondo, kuelekea nchini Ethiopia ili tusaidiane na wenzetu kwenye swala hili.

    Kinachowashangaza wengi ni vipi ndege hii aina ya Boeing 737 MAX 8 ilipata ajali haswa ikizingatiwa kuwa ilipokezwa taifa la Ethiopia miezi minne tu iliyopita. Ndio kitendawili ambacho kila mmoja anasubiri kiteguliwe na wataalam wa mitambo kutoka kampuni ya Boeing ambao wameanzisha uchunguzi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako