• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN asikitishwa na ajali ya ndege Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-03-11 09:00:52

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema katibu mkuu wa umoja huo Bw. Antonio Guterres, jana kwenye taarifa yake amesema amehuzunishwa na vifo vya watu vilivyotokea kwenye ajali ya kuanguka kwa ndege ya abiria iliyotokea jana karibu na Addis Ababa.

    Taarifa inasema Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa, wakiwemo wale wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Pia ametoa salamu za pole kwa serikali na wananchi wa Ethiopia.

    Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali ya Ethiopia, kuthibitisha wafanyakazi wa umoja huo waliofariki kwenye ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako