• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu Uingereza (EPL)- Liverpool yaitandika Burnley, Chelsea yavutwa shati, Arsenal yaendeleza ubabe

  (GMT+08:00) 2019-03-11 09:33:29

  Ligi kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea mwishoni mwa wikiendi, Livepool imeibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa ligi hiyo uwanja wa Anfield. Mabao ya Sadio Mane dakika ya 29 na 90 imewezesha Arsenal kutoka kifua mbele baada ya magoli mengine kufungwa na Roberto Firmino dakika ya 19 na 67.

  Mshambuliaji Mbelgiji Eden Hazard wa Chelsea ainusuru timu yake kupigwa nyumbani na Wolves baada ya kuifungia Chelsea bao la kusawazisha dakika ya 90 kufuatia Raul Jimenez kuanza kuifungia Wolves dakika ya 56 na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1.

  Arsenal imeibamiza Manchester United goli 2-0 uwanja wa Emirates mjini London na kumaliza rekodi ya kocha mpya Ole Gunnar Solskjaer kutofungwa kwenye ligi hiyo tangu achukue mikoba ya Jose Mourinho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako